Jeshi la Polisi Wilaya ya Wete Kas Pemba lapewa Wiki moja Uchunguzi tukio la Uchomaji Moto Baraza la Vijana Shehia ya GANDO
Mkuu wa wilaya
ya Wete Abeid Juma Ali ametoa muda wa wiki kwa jeshi la Polisi wilayani
humo kuhakikisha linakamilisha uchunguzi wa tukio la kuchomwa moto ofisi ya
baraza la vijana shehia ya Gando .
Haya ameyasema
wakati alipofanya ziara ya kutembelea eneo la tukio na kusema serikali ya
wilaya inalaani vika avikali vitendo hivyo ambavyo vimarudisha harakati za
kujikwamua na umaskini kwa vijana .
Amesema kuwa
serikali haiwezi kufumbia macho vitendo vya uhalifu vinavayofanywa na baadhi ya
wananchi ambao wanakwamisha juhudi za kujiletea maendeleo .
Naye Afisa
maendeleo ya vijana wilaya hiyo Seif Edward amewataka vijana kutovunjika moyo
kutoka na hujuma ambazo zimefanywa katika ofisi yao badala yake waendelee
kushirikiana .
Mmoja wa wajumbe
wa baraza la vijana shehia ya Gando Ahmed Said Khalfan amesema tukio hilo
limetokea majira ya usiku na limethiri ofisi yao pamoja na vifaa ambavyo
vilikuwa ndani yake.
Post a Comment