Header Ads

Ushahidi Kesi ya Ubakaji Mtoto Miaka 11 Waahirishwa Kusikilizwa Mahakama ya Mkoa wa Kas PEMBA, kutolewa Feb Mosi

Related imageMAHAKAMA ya Mkoa wa Kaskazini Pemba, imefunga ushahidi ya kesi ya kubaka inayomkabili Idrisa Ali Hamad (59) anaetuhumiwa kumbaka mtoto wa kike mwewnye umri wa miaka 11 huko nyumbani kwake Sellemu Wete.

Kesi hiyo inayosikilizwa na Mrajisi wa Jimbo Mahakama kuu Pemba Hussein Makame Hussein, imefunga ushahidi wa pande zote mbili, ambapo imepangwa kutolewa hukumu Febuari 1 mwaka huu.

Mahakama hiyo imesikiliza mashahidi wa wawili wa upande wa  mtuhumiwa pamoja na utetezi wake, ambapo mtuhumiwa huyo alikana kutenda kosa hilo na kukiri baadhi ya vipengele vya maelezo yaliyotolewa na mashahidi wa upande wa mlalamikaji, ikiwa ni pamoja na kukubali kumuita na kumtuma juisi mtoto huyo siku ya tukio kama ilivyoelezwa na shahidi namba tatu wa upande wa mlalamikaji.

"Mimi niliondoka kibanda majira saa 11.40 kuelekea nyumbani, kwa hiyo saa 11.30 lilipodaiwa kutokea tukio hilo sikuwepo nyumbani kwangu , lakini nilipofika nyumba nilimuona na nikamtuma mtoto huyo juisi " alidai mtuhumiwa.

 Jumla ya mashahidi wawili walifika mahakamani hapo kwa ajili ya kumtetea mtuhumiwa, ambapo wote walikiri kwamba walikuwa pamoja na mtuhumiwa siku ya tukio maeneo ya kibanda majira Sellemu Wete mara baada ya kuswali swala ya Alaasiri, ingawa walitofautiana muda walioachana na mtuhumiwa huyo.

Awali mtuhumiwa huyo, alidai aliondoka kibanda majira saa 11.40 kuelekea nyumbani kwake ambapo shahidi namba moja Said Suleiman Salim, alidai kuwa aliondoka maeneo hayo saa 11.20 na hakujua mtuhumiwa aliondoka muda gani katika eneo hilo.

Aidha shahidi namba mbili Zatia Hamad Hija alidai kuwa alifuatana na mtuhumiwa hadi kibanda majira wakati wanatoka msikitini na mara baada ya kufika katika eneo la kibanda majira , yeye   alianza kucheza karata na hakujua mtuhumiwa wakati alipoondoka hapo.

Mara baada ya kufungwa ushahidi, mwendesha mashitaka kutoka ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka Pemba, Ramadhan Suleiman Ramadhan aliiomba mahakama kutumia kifungu cha 301 (1) cha sheria namba 7 ya mwaka 2004 kinachompa mamlaka hakimu kutoa hukumu mara baada ya kufunga ushahidi, ombi ambalo lilikataliwa, ambapo hukumu ya kesi hiyo imepangwa kutolewa Febuari 1 mwaka.

No comments