SMZ Yaliliwa Utoaji wa Fidia Walioanguka Mikarafuni Zanzibar
Kamati ya fedha biashara na kilimo ya baraza la wawakilishi imeiomba Serikali kupitia wizara ya kilimo kuangalia upya kima cha fidia kinachotoa kwa watu walioanguka mikarafuu ili kwenda sambamba na gharama za kimaisha zinavyokwenda.
Katika kikao cha kuwafariji watu waliopata ajali ya kuanguka
mikarafu kilichofanyika katika ukumbi wa kiwanda cha makonyo Wawi Chakechake
mjumbe wa kamati hiyo ambaye pia ni mwakilishi wa jimbo la Mkwajuni Mh Ussi
Yahya Haji amesema wananchi wamekuwa wakitumia gharama kubwa kutafuta matibabu
baada ya kuanguka hivyo kuwepo kwa uwiano wa kifuta jasho kutasaidia upatikanaji
wa huduma bora kwa jamii hiyo.
Aidha mwenyekiti wa kamati hiyo na mwakilishi wa jimbo la
Fuoni mh Yussuf Hassan Iddi amesema Serikali inathamini mchango wa wananchi
wake kwa juhudi walioichukua ya kuliokoa zao la karafuu na ndio maana ikatoa
fidia hiyo kwa waliopata ajali ya kuanguka
Pamoja na hayo amelitaka shirika la Z S T C kuhakikisha imewapatia
kifuta jasho waliopata na ajali ya
kuanguka na kuharakisha kuwafanyia
taratibu za malipo kwa wale ambao wamechelewa maombi yao .
Nao baadhi ya watu waliopata ajali hiyo wamelishauri shirika
la Z S T C kuwa karibu na watu hao pale itakapo tokea ajali ya kuanguka ili
kutahisisha taratibu za maombi ya fidia zao.
Post a Comment