Wajumbe Mkutano mkuu NEC: Wana CCM Micheweni Endelezeni Mashirikiano kukijenga Chama Chetu
Katibu mwenezi wa CCM Wilaya ya Micheweni Abdallah Khamis Shaame akisisitiza jambo katika ziara ya viongozi wa CCM ya kuyatembelea majimbo ndani ya wilaya ya Micheweni. |
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Micheweni, Mariam Omar Ali akitoa maelekezo kwa viongozi wa Majimbo wakati wa Ziara hiyo katika Jimbo la Konde |
Baadhi ya viongozi wa CCM Wilaya ya Micheweni wakisikiliza Maelezo kutoka kwa Viongozi wa Jimbo la KONDE |
Mjumbe wa mkutano mkuu CCM Taifa, Bakar Hamis, akizungumza katika ziara hiyo |
Mjumbe wa mkutano mkuu CCM Taifa, Ramadhan Shaib, akisalimiana na Viongozi wa CCM jimbo la Konde wakati wa Ziara hiyo. |
Mjumbe
wa mkutano mkuu CCM Taifa, Kidawa Suleiman Khatib akisalimiana na Viongozi wa CCM jimbo la Konde wakati wa Ziara hiyo. |
Mjumbe wa mkutano mkuu CCM Taifa, Sophia Mzirai akisalimiana naViongozi wa CCM jimbo la Konde wakati wa Ziara hiyo. |
Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Micheweni, akisalimiana na Viongozi wa Kamati za siasa Jimbo la Konde |
Baadhi ya Viongozi wa Jimbo la Konde wakisikiliza Maelekezo kutoka kwa Katibu Mweneze CCM Wilaya ya Micheweni Abdallah Khamis Shaame wakati wa ziara hiyo Jimboni humo. |
CHAMA cha Mapinduzi CCM
wilaya ya Micheweni kimewataka wananchama wa chama hicho kuendeleza ushirikiano
ili kuondokana na makundi ndani ya chama kwa lengo la kuendelea kukijenga chama
na kuendeleza ushindi katika chaguzi mbalimbali.
Rai hiyo imetolewa na
wajumbe wa mkutano mkuu wa chama hicho NEC Taifa katika ziara ya kuwashukuru
wanachama wake kwa kuwachagua katika chaguzi zilizomalizika ndani ya chama
hicho.
Katika ziara hiyo
iliyoongozwa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Micheweni, Mariam Omar Ali wajumbe
hao wametembelea katika matawi ya jimbo la Konde na Tumbe wilayani humo.
Akizungumza na wajumbe
wa kamati za siasa CCM Jimbo la konde, Mwenyekiti wa CCM Wilaya amewataka
viongozi wa kamati za siasa kuhakikisha wanatekeleza wajibu wa wa kukitumikia
chama ikiwa ni pamoja na kuwaunganisha wanachama pamoja.
Alisema, “lengo la
chama chetu ni kuendelea kushinda katika chaguzi zote, kuanzia ngazi ya Wadi hadi
Taifa kwani ni wajibu wake kushinda, hivyo viongozi wa kamati za siasa munayo
kazi kubwa ya kuhakikisha azima ya Chama inaendelea kutimia.”
Kwa uoande wake mjumbe
wa mkutano mkuu CCM Taifa, Bakar Hamis nae amewataka viongozi waliochaguliwa
kufanya kazi na kuzitendea haki nafasi zao.
“Uchaguzi tumemaliza
kilichobakia sasa ni ni kufanya kazi na kama kulikuwa na makundi wakati wa
uchaguzi yafe na libakie kundi moja tu la wana CCM,” alisema Bakar
Aidha katika hatua
nyingine mu-NEC huyo alisema kuwa CCM imejipanga kuwajenga zaidi vijana ndani
ya Chama ili waweze kukiendeleza kwa nguvu zaidi na kuachana na siasa za
kuyumbayumba.
“Muda umefika kwa
wanaCCM kuachana na siasa za kuyumbayumba naomba viongozi hakikisheni munaandaa
taarifa halisi za wanachama hai waliopo ndani ya chama chetu,” aliongeza.
Nae Kidawa Suleiman
Khatib, amewashukuru wana CCM kwa kuwaamini na kuwapa nafasi ya kuwawakilisha
wanachama wa Micheweni katika Mkutano mkuu wa CCM Taifa na harakati za
kuendelea kukitunza chama katika misingi imara.
“Sisi viongozi wenu
tutakuwa msitari wa mbele kushirkianeni na nyie, lakini tunaombeni kama
kunasehemu mtaona mambo hayaendi sawa tukosoane kupitia vikao halali ndani ya
chama chetu,” alisema Kidawa.
Awali akifungua mkutano
huo Katibu mwenezi wa CCM Wilaya ya Micheweni Abdallah Khamis Shaame amewataka
matatibu wenezi wa matawi kurejesha hamasa kwa wanachama ili kuendelea
kukijenga chama katika kuelekea maadhimisho ya miaka 41 tangu kuanzishwa kwake.
Na Gaspary Charles
Post a Comment