Baba Miaka 59 Mbakaji wa Binti Miaka 11, Atupwa Jera Miaka Saba KAS PEMBA
HATIMAYE kesi ya ubakaji
iliyomuhusu Idrisa Ali Hamad (muki) 59 wa Sellem ya kumbaka mtoto wa kike
mwenye umri wa miaka 11 imefikia tamati baada ya mahakama ya mkoa kumtia
hatiani.
Akisoma hukumu
kwa mshitakiwa Mrajis wa Jimbo Mahakama Kuu Pemba Hassein Makame Hossein
amesema mahakama imeridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka na
hivyo kumwamuru aende chuo cha mafunzo kwa kipindi cha miaka saba pamoja na
kumlipa mwathiriwa fidia ya shilingi milioni mbili .
Kesi hiyo ambayo
ilikuwa imevuta hisia za watu ndani ya Mkoa wa Kaskazini Pemba , hasa baada ya
hakimu wa mahakama ya mkoa makame mshamba simgeni kujitoa kusikiliza hapo alifurika katika mahakama hiyo ili
kujua hatma na kesi hiyo .
Mapema mwendesha
mashtaka wa serikali ramadhan Suleiman ramadhan aliiomba mahakama kutoa adhabu
kali kwa mujibu wa sheria ili iwe fundisho kwake na wengine na kudai kwamba
matendo hayo yanazidi kushamiri siku hadi siku .
Akitoa utetezi
mahakamani hapo wakili wa mshitakiwa mohammed ali aliiomba mahakama impunguzie
adhabu mteja wake imtoze faini badala ya kifungo kwani sheria inakubaliana na
hilo huku akidai kwamba mteja wake anasumbuliwa na magonjwa mbali mbali ikiwemo
kisukari , presha na figo.
"Naiomba
mahakama impunguzie adhabu mteja wangu ikiwa ni pamoja na kumtoza faini
badala ya kifungo kwani sheria inakuliana na hilo , na pia mteja wangu
anasumbuliwa na ugonjwa wa presha , figo na kisukari " alieleza.
Hukumu
hiyo imepokelewa vyema na baadhi ya wananchi ambao wameelezea
kuridhishwa na hatua hiyo kwani kesi hiyo imechukua muda mfupi hadi
kutolewa uwamuzi wake.
"Hivi
ndivyo tunavyotaka , kesi ikifikishwa mahakamani ishughulikiwe haraka
na wananchi watajenga imani na chombo cha mahakama ambacho kinakazi ya
kutafsiri sheria " alisema Katibu Tawala Mkoa Ahmed Khalid Abdalla .
Muki
alitenda kosa hilo disemba 2 /2017 , huku nyumbani kwake Sellem
majira ya saa kumi na moja na nusu za jioni ambapo jumla ya mashahidi
sita kwa upande wa mashitaka walitoa ushihidi wao huku mashahidi wawili
walifikia kutoa ushahidi wa upande wa mshitakiwa .
Post a Comment