Wakamatwa na Vifurushi 25 vya Bangi KAS PEMBA
WATU wawili wakaazi wa Mkoa wa Tanga
wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba baada ya kukamatwa
wakiwa na mafurushi ishirini na tano (25) ya majani makavu
yanayosadikiwa kuwa ni bangi yenye uzito wa kilo tano na nusu.
Wawili hao ambao wako chini ya ulinzi wa Polisi
la Polisi ni Seif Yussuf Msumari pamoja na Shadia Stephano wako wakaazi wa Mkoa
wa Tanga.
Akizungumza ofisini kwake Kamanda wa Polisi Mkoa
wa Kaskazini Pemba Kamishna msaidizi Haji Khamis Haji amesema watuhumiwa hao
wamekamatwa na askari katika eneo la bandari ya wete.
Amesema kuwa jeshi la polisi bado linaendelea
kuwahoji watuhumiwa na upelelezi ukikamilika watfikishwa mahakamani kujibu
tuhuma ambazo zinawakabili .
“Kwa sasa tunaendelea kuwahoji na upelelezi
ukikamilika watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma ambazo zinawakabili ”
alifahamisha.
Amesema kwa upande wa Jeshi la polisi wamejipanga
kuendesha misako na operesheni sehemu za bandari , madago pamoja na maeneo
mengine yanayodhaniwa kutumika kupitisha dawa za kulevya ili kuweza kutimiza
lengo la kutokomeza biashara haramu ya dawa za kulevya.
“Hizi operesheni tunazoendelea nazo ni endelevu ,
lengo ni kuhakikisha wananchi wanaishi salama bila ya kutumia dawa za kulevya ”alieleza
Kamanda.
Aidha kmanda haji amewataka wananchi kuendelea
kushirikiana na jeshi la polisi kwa kutoa taarifa sahihi ambazo zitafanikisha
kuwakamata wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya .
Amesema jeshi la polisi linahitaji ushirikiano
kutoka kwa wananchi pamoja na vikosi vyengine vya ulinzi katika kufanikisha
azma ya kukabiliana na biashara hii , hivyo ni vyema kila mmoja akatambua
kwamba vita ya dawa za kulevya ni ya wote.
Post a Comment