Katibu Mkuu wa UN atoa wito wa kusimamisha mapigano Syria
Katibu Mkuu wa Umoja wa
Mataifa Antonio Guterres jana ametoa wito wa kusimamisha mara moja mapigano
katika eneo linalokaliwa na waasi la Ghouta Mashariki nchini Syria.
Bw. Guterres amesema hayo
kwenye kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, ambapo ameeleza
kusikitishwa kwake na mateso makali wanayopata raia wanaoishi kwenye eneo hilo.
Amezitaka pande zinazopingana kwenye eneo hilo kusimamisha mapigano na kuruhusu
misaada ya kibinadamu kuwafikia wahitaji na kuruhusu kuondolewa kwa watu 700
wanaohitaji matibabu ya haraka ambayo hayaweze kupatikana katika eneo hilo.
Wakati huohuo, Bw. Guterres
amerejea tena umuhimu wa mitazamo ya kivitendo katika kuzuia badala ya
kukabiliana na migogoro. Amesema kuzuia migogoro ni wajibu wa msingi wa nchi
wanachama wa Umoja wa Afrika, na kwamba Umoja huo uko tayari kusaidia nchi hizo
kutatua migogoro yao na kuzuia kutokea kwa machafuko.
Post a Comment