Zambia yatarajia ukuaji mzuri wa uchumi mwaka huu
Serikali
ya Zambia imesema, uchumi wa Nchi hiyo unatarajiwa kukua vizuri mwaka huu
kutokana na kuwepo kwa mazingira tulivu ya kiuchumi.
Waziri
wa fedha wa ZAMBIA Bibi MARGARET MWANAKATWE amesema, matarajio hayo yanatokana
na utekelezaji wa sera mbalimbali, na mageuzi ya kimfumo na kisheria chini ya
mradi wa Serikali wa kutuliza uchumi na ukuaji.
Amesema
ukuaji wa uchumi unatarajiwa kuwa mzuri huku mfumuko wa bei ukipungua na urari
wa kifedha ukidhibitiwa ndani ya Bajeti.
Lakini,
Bibi MWANAKATWE pia amesema, mabadiliko ya hali ya hewa na kiwango cha juu cha
mikopo vitatoa athari hasi kwa shughuli za kilimo na uzalishaji wa umeme.
Post a Comment