'Kifafa Cha Mimba Kinatibika' - Dk SALEH
MAMA
wajawazito wametakiwa kuwahi vituo vya Afya na hospitali kwa ajili ya
kupata ushauri wa kitaalamu wanapobaini kuwa ni wajauzito ili kujikinga
na Maradhi mbalimbali ikiwemo Kifafa cha Mimba .
Akizungumza
na REDIO JAMII huko Ofisini
kwake Daktari wa masuala ya Uzazi katika Hospitali ya WETE Dr HAWARA SALEH amesema Kuwahi
kwenye vituo vya afya na Hospitali kunaweza pia kumkinga mama dhidi ya
kifafa cha mimba ambacho kinachangia kupoteza maisha ya mama na mtoto.
Dk. SALEH
amesema kwamba kifafa cha mimba kinatibika iwapo mama atawahi Kliniki baada ya
kubaini kwamba ana ujauzito.
Aidha Dakitari
huyo amezitaja dalili za Ugonjwa wa Kifafa cha Mimba na kuwataka akimama
wanapohisi wanadalili hizo kuwahai hospitali .
Post a Comment