'UNGA' Wampeleka Jela Miaka Mitatu PEMBA
MAHAKAMA
ya Wilaya ya Wete ,chini ya hakimu wa mahakama hiyo ABDALLA YAHYA SHAMHUNA ,
mwendesha mashtaka wa Serikali JUMA ALI JUMA imempeleka chuo cha mafunzo kwa
kipindi cha miaka mitatu au kulipa faini ya shiingi milioni tano kijana
SULEIMAN ALI SALEH baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kupatkana na dawa za
kuelevya.
Hati
ya mashitaka inaeleza kwamba kijana huyo ametiwa hatiani kwa kosa la kupatikana
na dawa za kuevya aina ya hereoin kete nne zenye uzito wa gramu 0.06 .
Kijana
SULEIMAN ameshindwa kulipa faini ya shilinga milioni tano na ameanza maisha
mapya akiwa ni mwanafunzi wa Chuo cha Mafunzo akitumikia adhabu ya Miaka
mitatu.
Post a Comment