Header Ads

Ahukumiwa Wiki mbili kwa Tuhuma za Dawa za Kulevya



Image result for mahakama 
MAHAKAMA ya Mkoa wa KASKAZINI PEMBA imempeleka rumande wa kwa kipindi cha wiki mbili ,KOMBO SALIM BAJAKA (40) baada ya kufikishwa mahakamani hapo akikabiiwa na tuhuma ya kupatikana na unga unaodhaniwa kuwa dawa za kulevya aina ya herion

Imedaiwa  mahakamani hapo na mwendesha mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka wa Serikali RAMADHAN SULEIMAN RAMADHAN , mbele ya hakimu wa MAHAKAMA hiyo MAKAME MSHAMBA SIMGENI kwamba mtuhumiwa huyo amekamatwa februari 12 /2018 .

Kwa Mujibu wa hati ya mashtaka inaeleza kwamba siku ya tukio majira ya saa 11:50 jioni  huko MTEMANI , mtuhumiwa huyo alipatikana na unga unaodhanikiwa kuwa dawa za kulevya wenye uzito wa gramu 1.81 jambo ambalo ni kosa kisheria.

Baada ya kusomewa shitaka lake mtuhumiwa amekana kosa na amepelewa rumande hadi machi 8 /2018 kesi hiyo itakapokuja kutajwa tena .

No comments