Header Ads

ZAWA Kudai Bili ya Maji Taasisi za Serikali , DC WETE atoa Agizo



Image result for mabomba ya maji 

SIKU moja baada kutolewa taarifa ya uwepo na taasisi za Serikali ambazo hazichangii  huduma ya Maji, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji -ZAWA -PEMBA  OMAR MSHINDO BAKAR amekiri kuwepo  Taasisi   za Serikali ambazo  zinadaiwa na Mamlaka hiyo .

Amesema   kushindwa kuchangia huduma ya maji kwa baadhi ya taasisi hizo kume sababisha Mamlaka kutotekeleza majukumu  yake ya kuifanya huduma hiyo kuwa  endelevu .

Akizungumza na REDIO JAMII MICHEWENI, Mshindo amesema  iwapo taasisi hizo zitaweza kuchangia ipasavyo , mamlaka  itaweza kutoa huduma  bora ikiwa ni pamoja na kuifanyia marekebisho mindombinu inayosambaza maji .

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya WETE , ABEID JUMA ALI  amelazimika kufanya ziara katika ofisi ya Mamlaka na kuagiza   kuorodheshwa majina ya taasisi ambazo zinadaiwa kuwasilisha majina ofisini kwake kuwa si zaidi ya jumatatu wiki ijayo.

Hata hivyo bado amesema kuwa wanaendelea kufuatilia suala hilo ili kujua taasisi hizo zinadaiwa fedha  kiasi gani na Mamlaka hiyo.
Na Masanja Mabula

No comments