Dumu la Maji WETE lauzwa TSH 1,000, Wananchi Wahaha
UKOSEFU wa huduma ya maji Safi na Salama kwa baadhi ya maeneo ya mji wa WETE umeifanya huduma hiyo kuwa adimu ambapo wananchi wanalazimika kununua dumu moja la maji kwa shilingi 1000.
Baadhi ya maeneo ya mji wa WETE
yaliyotebelewa REDIO JAMII MICHEWENI umebaini kuwepo na adha kubwa wanayoipata
kuifatuta huduma hiyo masafa marefu .
Wakizungumza kwa masikitiko baadhi ya
Wananchi wa Mji huo wamesema ukosefu wa huduma hiyo umesababisha kutumia Muda
mwingi kuifuta mabondeni huku wakichelewa kufika ofisini pamoja na wanafunzi
kuchelewa skuli .
Aidha wameiomba mamlaka ya maji ZAWA
kuliangalia suala hilo kwa jicho la huruma ili kuwaondeshea tatizo hilo .
Kwa
upande wake afisa wa mamlaka ya Maji ZAWA Mkoa wa KASKAZINI PEMBA BARAKA ALI
MBWANA amesema tayari Mamlaka inaendelea na jitihada ya kufanyia matengenezo Bomba
lililopasuka na huduma hiyo itarejea ndani ya kipindi cha siku mbili.
Na Masanja Mabula
Post a Comment