Header Ads

Elimu ya Ujasiriamali Kuwanufaisha Wachimba Mawe Wilaya ya MICHEWENI



Image result for mawe 
WACHIMBAJI wa Mawe na wavunjaji wa Kokoto Wilaya ya MICHEWENI Mkoa wa KASKAZINI PEMBA  wanatarajia kunufaika na Elimu ya Ujasiriamali , ambayo itawasaidia kujiepusha na vitendo vya uharibifu wa mazingira .

Elimu hiyo itawaweza  kutafuta njia mbadala ya kiuchumi na kuacha kutegemea kazi ya uchimbaji wa  mawe na uvunjaji wa kokoto kama eneo pekee ambalo linaweza kutumiwa na wachimbai hao kwa ajili ya kuendesha maisha yao na familia zao.

Wachimbaji hao ambao wengi wao ni vijana na watoto  , wanadaiwa kusababisha ardhi  iliyokuwa inatumika kwa ajili ya kilimo yameathirika  kutokana na shughuli hizo  na hivyo kutokuwa mazuri kwa kilimo .

Wakizungumzia ushauri huo , Wananchi wanaojihusisha na uchimbaji wa mawe na uvunjaji wa kokoto katika eneo hilo wameiomba Serikali kuwapa muda wakati ikiendelea kuwatafutia eneo jengine kwa ajili ya kujikumu kimaisha.

Mmoja wa wachimbaji wa mawe aliyefahamika kwa jina ZUME KOMBO amesema pamoja na uwamuzi huo wa Serikali lakini iko haja kuhakikisha wanapatiwa elimu ambayo itawasaidia kushiriki kuhifadhi mazingira.

Akizungumza na wachimbaji hao Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba OMAR KHAMIS OTHMAN  amesema Serikali inaendelea kutafuta mbinu mbadala ambazzo zinaweza kutumiwa na vijana wakati alipofanya ziara ya kutembelea maeneo hayo katika eneo la Mkwaju Mgoro Micheweni .

‘’Serikali inampango wa kuwatafutia mradi badala ili muweze kuendesha shughuli zeni kiuchumi ikiwa kuwapatia elimu ya ujasiriamali ’’alieleza.

Aidha Mkuu wa Mkoa pia ametumia fursa hiyo kuwaasa wachimbaji wa mawe na uvunjaji wa kokoto kuwa na utaratibu wa kufukia mashimbo pamoja na kupanda miti ya biashara na matunda ili kuifanya ardhi irejee kwenye uhalisia wake .

Naye katibu Tawala Mkoaa huo AHMED KHALID ABDALLA amewashauri wachimbaji hao kujiunga kwenye vikundi vyaa ushirika ili waweze kunuifaka na huduma za mikopo kutoka taasisi ambazo zinatoa mikopo kwa wajasiriamaali.

Ahmed amesema Serikalai imeandaa  mazingira mazuri kwa wajasiriamali wadogo na wakati , hivyo na kuwashauri kuchangamkia fursa ambazo zimewekwa kwa ajili kukuza kipato chao .

‘Serikali zote mbili zimeweka mazingira mazuri kwa wajasairiamali , hivyo mnatakiwa kujiunga akwenye vikundi vya ushirika vya uzalishaji mali ili muweze kujipatia mikopo ’’alisisitiza.

 Afisa Mkuu wa Mamlaka ya usimamizi wa mazingira Pemba  ABUBAKAR ALI amewataka vijana hao kuangaliwa uwezekano wa kufukia mashimo ili kuirejesha ardhi katika uhalisia wake.
Na Masanja Mabula

No comments