RC KAS PEMBA aahidi Kuendelea Kutangaza Maeneo ya Utalii Kwa Wawekezaji
Mkuu
wa Mkoa Kaskazini Pemba Mhe. Omar Khamis Othman amesema serikali ya Mkoa itaendelea
kuyaibua, kuyaendeleza na kuyatangaza maeneo ya Utalii ili yaweze
kutumika kwa ajili yakukuza pato la nchi.
Akizungumza
na ujumbe wa Makamishna wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar huko Ofisini kwake,
Mkuu huyo wa Mkoa amesema Serikali imeyaibua maeneo mengi na kuyatangaza
ambayo kwa sasa yamekuwa ni kivutio cha watalii wanaokuja kuyatembelea.
Amesema
lengo la Serikali ya Mkoa kuyaibua , kuyaendelea na kuyatangza maeneo hayo ni
katika kuunga mkono kauli mbinu ya Serikali kuu ya kuhimiza dhana ya Utalii kwa
wote.
‘Serikali
ya Mkoa inaendelea kuyaibua na kuyatangza maeneo ya utaii ili wananchi waweze
kuyatambua na kuyalinda pamoja na kuyatumia kwa ajili ya kutimiza adhama ya
Serikali ya Utalii kwa wote’’ alifahamisha.
Aidha
Mkuu huyo wa Mkoa ameitaka Mamlaka ya Uwekezaji na Vitenga Uchumi ZIPA kuondoa
vikwazo kwa wawekezaji wanaotaka kuwekeza miradi ya utalii katika maeneo
yaliyotengwa na Serikali .
Amebainisha
kwamba wapo baadhi ya wawekezaji ambao kwa mujibu wa taratibu
wametimiza vigezo vya kuwekeza miradi yao , lakini wanapokewa vikwazo kutoka
ZIPA jambo ambalo linatakiwa kuangaliwa na Kamisheni ya Utalii.
Akizungumza
kwenye kikao hicho Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar Vuai
Iddi Lila amesema Sekta ya Utalii imekuwa na mchango Mkubwa katika kuchangia
kipato cha nchi.
Lila
ameiomba Serikali ya Mkoa kuwaelimisha wananchi wanaoishi kwenye maeneo ya
ukanda wa uwekezaji kutambua faida na utalii kwa maendeleo ya ukuaji wa
uchumi wa nchi na mwananchi mmoja mmoja.
‘Sekta
ya Utalii imekuwa ikichangia ukuwaji wa pato la Taifa na mwananchi mmoja mmoja
kwani ndiyo Sekta pia inayotoa ajira kwa vijana ’’alieleza Lila.
Nae
Katibu Tawa wa Mkoa huo Ahmed Khalid Abdalla ameitaka Kamisheni hiyo kuboresha
huduma za miundo mbinu katika maeneo ya uwekezaji.
Amesema
yapo maeneo ambayo wawekezaji wamewekeza lakini bado yanakabiliwa na
miundombinu mibovu hususani ya barabara , na kwamba yanahitaji kuboreshwa na
kurahisha usafiri wa wananchi.
‘Mkoa
wa Kaskazini Pemba unamaeneo mengi ya ukanda wa Utalii ,ikwemo Makangale lakini
bado miundombinu ya barabara inakwamisha maendeleo ya sekta hii ’’alieleza.
Hata
hivyo mmoja wa makamishina Kamisheni hiyo alieleza kwamba ukarabati wa barabara
kuelekea Makangale unatarajia kuanza mwezi machi kwa kiwango cha kifusi .
Post a Comment