Watu 250 wauawa Ghouta wakiwemo Watoto
Idadi ya watu waliokufa katika
mashambulizi ya anga yanayotekelezwa na vikosi vya serikali huko huko Ghouta
mashariki imefikia 250 ambapo kati ya idadi hiyo 50 wakiwa ni watoto.
Umoja wa mataifa nchini Syria umesema
una mashaka makubwa juu maisha ya mamia ya raia ambao bado wapo katika eneo
linalolengwa na mashambulizi ya anga ya vikosi vya serikali ya Syria katika
eneo la Ghouta mashariki.
Mashambulizi hayo yaliyoanza siku ya
jumapili bado yanaendelea na kusababisha vifo na majeruhi wengi wakiwemo
watoto.
Umoja wa mataifa umeelezea mashaka yake
juu ya kutokea Allepo nyingine,ambapo ukombozi wa mji huo mwaka 2016 pia
ulisababisha vifo vya mamia ya raia kufuatia mashambulizi ya vikosi vya
serikali.
Geert Cappelaere afisa kutoka UNICEF
ameiambia BBC kuwa watoto ni miongoni mwa waliouawa
Idadi ya watu waliokufa ndani ya siku
mbili ya mashambulizi hayo imepanda na kufikia 250 kwa mjibu wa ripoti kutoka
Ghouta mashariki karibu na mji mkuu Damascus,huku kati yao 50 wakiwa ni watoto.
Post a Comment