Mtanzania akamatwa na dhahabu ya $1m Nairobi
Maafisa wa forodha nchini Kenya
wamemkamata mwanamume anayedaiwa kuwa raia wa Tanzania katika uwanja wa
kimataifa wa ndege wa Jomo Kenyatta, Nairobi akisafirisha dhahabu ya thamani ya
dola milioni moja, taarifa zinasema.
Mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 46
anadaiwa kuwasili kutoka Mwanza, Tanzania kupitia uwanja wa Kilimanjaro na
alikuwa safarini kuelekea Dubai.
Gazeti la kibinafsi ya Nation linasema
mwanamume huyo, ambaye jina lake halijafichuliwa kufikia sasa, aliwasili uwanja
wa JKIA Ijumaa 16 Februari akiabiri ndege ya Precisio Airlines na alitaka
kuabiri ndege ya Kenya Airways kuelekea Dubai.
Maafisa wa uIdara ya Uchunguzi wa Jinai
wakiandamana na maafisa wa uchunguzi kutoka Mamlaka ya Mapato ya Kenya (KRA)
walimhoji na akaandikisha taarifa.
Sheria za Usimamizi wa Forodha za
Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) za mwaka 2004, kKifungu 85(3) na Kiambatisho
cha Pili Sehemu B (4) huharamisha usafirishaji wa madini ambayo hayajapitia
viwandani katika kanda ya Afrika Mashariki.
Vipande hivyo vya dhahabu vya uzani wa
kilo 32.3 vinashikiliwa na maafisa wa idara ya forodha wa KRA huku uchunguzi
zaidi ukiendelea.
Chanzo: BBC Swahili
Post a Comment