'Wafanya Biashara Fuateni Taratibu Ukataji wa Leseni'- KAMISHENI YA UTALII ZANZIBAR
KAMISHENI ya utaii zanzibar imewataka wafanyabiashara kufuata taratibu za ukataji wa Lessi za Biashara zao ili kuwaweza kuendesha Biashara zao bila ya usumbufu.
Mwanasheria
wa kamisheni hiyo Bi VIWE ISSA MAKAME amesema biashara yoyote inayotoa huduma
za wageni , hiyo inatakiwa kukatiwa leseni kutoka kamisheni ya utalii .
Akizungumza
na REDIO JAMII MICHEWENI katika Hoteli ya MANTA RESORT, Wilaya ya Micheweni, Mkoa wa Kasikazini Pemba, Bi Viwe amesema
kamisheni imebaini kuwepo na wafanyabiashara wa migawa inayohuduma wageni
kutumia leseni kutoka Halmashauri jambo ambalo sio sahihi kisheria.
Aidha
amesema mtu yoyote ambaye atabainika kufanya Biashara bila ya kuwa na leseni ya
Kamisheni ya utalii atatozwa faini kwa mujibu wa Sheria .
Post a Comment