Mamlaka ya Maji ZAWA Kisiwani Pemba yapewa Somo Jipya
Mwenyekiti
wa bodi ya Mamlaka ya Maji ZANZIBAR (ZAWA) Dr ZAKIA MOH’D ABUBAKAR ameitaka Mamlaka
ya Maji Kisiwani Pemba kuzidisha kasi ya kuwapatia wananchi huduma hiyo kwa
kiwango kikubwa licha ya kuwepo changamoto za hapa na pale zinazoikabili
mamlaka hiyo.
Amesema
upatikanaji wa maji katika kisiwa hicho unaridhisha japo makusanyo ya malipo ni
madogo ukilinganisha na asilimia 80% ya huduma inayotolewa kwa wananchi wa
huko.
Dr
ZAKIA ameyasema hayo huko kituo cha huduma ya maji Taifu Wete mara baada ya
kumaliza ziara ya kuangalia hali ya upatikanaji wa
maji safi na salama kisiwani
Pemba .
Pamoja
na changamoto hiyo Mwenyekiti huyo ameitaka (ZAWA) Pemba kutosita kuwafikishia
maji wale ambao hawajapata huduma hiyo kwa sasa
Naye
Mkurugenzi wa Mamlaka ya maji (ZAWA) Pemba OMAR MSHINDO BAKAR amesema wananchi wanapaswa kuiamini mamlaka hiyo wakati wa wanapohudumiwa
na kuwataka kuichangia ili kuwa yenye ubora zaidi .
Awali
mjumbe wa bodi hiyo BAKAR ASSAD ameutaka uongozi wa (ZAWA) Pemba kuandaa mkakati
maalumu wa utekelezaji unaoweza kuendeleza miradi ya maji kuwa
Na Juma Mussa Pemba
Post a Comment