Walimu waonywa kuweka Mikakati Bora kuimarisha Ufaulu kwa Wanafunzi WETE
Mkuu wa Wilaya ya Wete ABEID
JUMA ALI amewataka Walimu wa Skuli ya Sekondari MITIULAYA
kushirikiana na kamati ya skuli pamoja na wazazi wa wananfunzi ili
kuweka mikakati iliyo bora itakayopelekea wanafunzi kufanya vizuri katika
mitihani yao.
Kauli hiyo ameitowa
wakati alipokuwa akizungumza na walimu huko katika ukumbi wa ofisi ya Mwalim
Mkuu Sekondari MITIULAYA Wete Mkoa wa KASKAZINI PEMBA.
Amesema matokeo mazuri
hupelekea sifa kwa walimu hivyo ni vyema kuwajibika ipasavyo na kuweka mikakati
imara ambayo itapelekea wanafunzi kutojiingiza katika vitendo
viovu vinavyosababisha kutofanya vizuri katika masomo yao.
Kwa upande wake Mwalim Mkuu
wa Skuli hiyo Bi RIZIKI MAKAME FAKI ameahidi kwamba walimu hao
watatekeleza majukumu yao ya kazi ipasavyo ili kuhakikisha
wanapasisha wanafunzi wengi katika skuli hiyo.
Hata hivyo amesema
changamoto inayowakabili katika Skuli hiyo hadi kupelekea kutofanya
vizuri katika mitihani yao ni kwamba baadhi ya wazazi na walezi hawataki
kutoa ushirikiano wao na kupelekea Wanafunzi wengi kuwa wtovu wa nidhamu pamoja
na kukosa mwalimu wa somo la Sanyansi na somo hilo kushindwa kusomeshwa .
Na Khadija Mahmoud Pemba.
Post a Comment