Header Ads

Wanafunzi wa Kike Wilaya ya Micheweni Hatarini Kuozeshwa


Related image
PICHA NA MAKTABA

 WIMBI la wanafunzi kuacha masomo na kuolewa katika Wilaya ya MICHEWENI, Mkoa wa KASKAZINI PEMBA linaonekana kushika kasi katika siku za hivi karibuni.
Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na kituo cha REDIO JAMII MICHEWENI umebaini kuwepo na idadi kubwa ya wanafunzi ambao huenda wakakatishwa masomo na kuolewa na hivyo kusitisha ndoto zao za baadaye.
Taarifa za awali ambazo redio jamii imezipata na inaendelea kukusanya takwimu, zinaeleza kwamba tatizo la kukatishwa masomo wanafunzi linachangiwa na wazazi na walezi ambao wameshindwa kutoa kipaombele cha elimu kwa mtoto wa  kike
Pia uchunguzi huo umebaini kwamba wanafunzi wanaocha masomo na kuolewa ni wale wanaosoma skuli za Sekondari.

No comments