WANAHABARI WATAKIWA KUZINGATIA MAADILI
Waandishi
wa habari nchini wametakiwa kuzingatia maadili ya taaluma yao wanapotekeleza
majukumu ili kuepusha migogoro katika jamii.
Wito
huo umetolewa leo mjini Dodoma na Mwezeshaji ROSE MWALIMU katika Mafunzo ya
kuwajengea uwezo waandishi wa Habari vijijini
kuandaa vipindi bora yanayoendeshwa na Shirika la Elimu, Sayansi na
Utamaduni-UNESCO-.
Amesema
kutozingatia maadili kama vile ukweli na vyanzo sahihi kutasababisha vyombo
vyao kutoaminika na Jamii husika.
Waandishi
wa habari 49 kutoka Redio za jamii 24 nchini wanashiriki mafunzo hayo ya siku
saba ambayo yameanza Februari 06, hadi Februari 12 Mwaka huu.
Post a Comment