Header Ads

'Wazazi hakikisheni Watoto wenu Wanaenda Skuli' DC MICHEWENI



Wazazi Na Walezi Wilaya Ya Micheweni Wametakiwa Kuwasimamia Watoto Kusoma Kwa Bidii Ili Kuweza Kufanikisha Masomo Yao Vizuri
Ushauri Huo Umetolewa Na Mkuu Wa Wilaya Ya Micheweni SALAMA MBARUKU KHATIBU Wakati Alipokuwa Akizungumza Na Wazazi Ambao Wana watoto Wanaotarajiwa Kufanya Mitihani Ya Kitafa
Amesema Wazazi Na Walezi Watakapo Wasimamia Watoto Wao Kusoma Wanaweza Kufaulu Kwa Asilimia Kubwa Na Kuweza Kupata Wataalamu  Wa Kada Mbali Mbali
Salama Amesema Yuko Tayari Kuchangia Kwa Njia Ya Aina Yeyote Ile Ili Kuweza Kufanikisha Suala La Elimu Katika Wilaya Hiyo
 Naye Mwalimu Mkuu Wa Skuli Ya Micheweni Sekondari ISIMALI ALI Amesema Walimu Wamekuwa Wakiachiwa Mzigo Pekeyao Jambao Ndio Linalosababisha Kutofaulu Vizuri Wanafunzi Wao
Amesema iwapo Wazazi Na Walezi Watakuwa Na Moyo Wa Kushirikiana Na Walimu Basi Wanafunzi Wa Wilaya Ya Micheweni Watakuwa Nikioo Cha Wilaya Nyengine
Hata Hivyo Wazazi Na Walezi Nao Wamesema Wao Wako Tayrai Kushirikiana Na Walimu Kwani Waliachiwa Mzigo Muda Mkubwa Na Sasa Wao Ndio Watakao Simamia Watoto
Wamesema Hapo Awali Walikuwa Hawashirikishwi Katika Maswali Ya Elimu Na Wao Wakaona Kama Hawahusika Katika Kusimamia Watoto Wao Katika Maswali Ya Kielimu
Na Ali Masoud Kombo

No comments