Maradhi ya Mripuko 'Kufagia' Wanafunzi 1,622, Sikuli ya UONDWE Kisiwani Pemba
WANAFUNZI
wa Skuli msingi Uwondwe Shehia ya Mtambwe , wako hatarini kupata maradhi ya
mripuko iwapo hatua za haraka hazitachukuliwa kulipatia ufumbuzi tatizo la
upungufu wa matundu ya vyoo skulini hapo.
Skuli
hiyo kongwe kisiwani Pemba yenye wanafunzi 1622 , ina jumla ya matundu ya vyoo
matatu yaliyojengwa kabla ya Mapinduzi ambayo kwa sasa yanahatarisha usalama wa
wanafunzi .
Mwalimu
mkuu wa skuli hiyo Khadija Said Khalfan amemwambia Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini
Pemba kuwa uongozi wa skuli umelazimika kuzuia matumizi ya vyoo ambavyo
vimejengwa kabla ya mapinduzi , na hivyo kuwafanya baadhi ya wanafunzi
kujisaidia kwa kutumia vichaka vilivyojirani na skuli
“Tuna
matundu matatu ya vyoo , na idadi ya wanafunzi ni 1622 wakiwemo watoto wadogo
wa maandalizi , hivyo hulazimika kutumia vichaka jambo ambalo linahatarisha
usalama wa maisha ya wanafunzi ”alieleza.
Picha na Maktaba |
Akizungumzia
suala la upasishaji wa wanafunzi , Khadija amesema sio mzuri na kutaka tatizo
la upunguzu wa walimu ni sababu ya matokea mabaya katika skuli hiyo .
Amesema
kuwa iwapo changamoto hiyo itapatiwa ufumbuzi , matokeo ya wanafunzi yatakuwa
mazuri kwani walimu watakuwa na muda wa kutosha kupitia masomo ya wanafunzi.
Naye
Mkuu wa mkoa wa Kaskazini Pemba Omar Khamis Othman ambaye amefanya ziara
ya kushtukiza skulini hapo , ameeleza kusikitikishwa na kitendo cha wakaazi wa
shehia hiyo kuyaziba baadhi ya matundu ya vyoo
.
Amesema
kitendo hicho ambacho kimefanywa na wananchi wa Mtambwe kinapaswa kulaaniwa na
kila mpenda maendeleo kwani kinarudisha nyuma harakati za Serikali za kuboresha
kiwango cha elimu.
“Kwa
mtu mwenye imani na mpenda maendeleo hawezi kufanya kitendo kama hicho kwani
kuziyaba matundu ya vyoo kunawafanya wanafunzi watumie vichaka , ambapo kwa
kipindi cha mvua ni hatari wa usalama wa watoto ”alisisitiza.
Aidha
Mkuu wa Mkoa ameahidi kuzungumza na wananchi wenye asili ya Mtambwe
kuwashawishi kusaidia maendeleo ya skuli hiyo .
“Mtambwe
ina vijana wengi wasomi na wanasiasa wazuri , lakini wameshindwa kujitokeza
kusaidia maendeleo ya skuli yao , kwa hivyo Serikali ya Mkoa itafanya juhudi
kuwatafuta na kuwashawishi kusaidia kuzipatia ufumbuzi tatizo hili ”alisema .
Sheha
wa Shehia ya Mtambwe Kaskazini Bakar Suleiman Khamis amesema licha ya
Mwakilishi wa Jimbo la Mtambwe Khadija Kibano kuishi umbali usio zidi mita mia
tano kutoka ilipo skuli , lakini ameshindwa kutembelea na kuangalia matatizo
yaliyopo.
Skuli
ya Uwonde imejengwa mwaka 1934 , inakabiliwa na changamoto pia ya upungufu wa
walimu ambapo kwa sasa inajumla ya walimu 19 na vyumba vya madarasa 22.
Na Masanja Mabula
Post a Comment