Vijana Kisiwani Pemba wanufaika na Elimu ya Utawa Bora
Vijana wa Mkoa wa Kaskazini
Pemba wametakiwa kushiriki katika shughuli za mandeleo ili Taifa kuweza kupiga
hatua.
Ushauri huo
umetolewa na MWANAID ALI SAID Kutoka shirika la ACTION AID wakati alipokuwa
akitoa mafunzo juu ya utawala bora na ushirikishwaji katika ukumbi wa Jamhuri
Wilayani Wete.
Amesema kuwa
wameamua kuwasaidia vijana kwa kuwapatia mafunzo ya utawala bora na
ushirikishwaji ili kuweza kujua wajibu wao ndani ya serikali na jamii kwa
ujumla.
Akizungmza katika
mafunzo hayo mjumbe kutoka shirika la umoja wa Mataifa UN, Mohamed Hassan Ali
amesema Uwazi na ushirikishwaji ndiyo chanzo cha kuwepo kwa utawala bora katika
Taifa.
Ali amesema bado
kuna changamoto kwa baadhi ya vijana ambao wanajiingiza katika masuala la
kisiasa kutokana na wengi wao kutokuwa na elimu ya kutosha juu ya siasa.
Nao baadhi ya
vijana walioshiriki mafunzo hayo wamesema kuwa mafunzo hayo waliyoyapata kutoka
shirika hilo yamewasaidia kutambua wajibu na mchango wao katika Taifa.
Mafunzo hayo ya
siku mbili ya kuwajengea uwezo vijana juu ya dhana ya utawala bora na ushirikishwaji
yanajumuisha jumla ya vijana 25 kutoka mkoa wa kaskazini Pemba.
Post a Comment