Shehia NNE Jimbo la Micheweni Kunufaika na Mfuko wa Mwakilishi
KAMATI ya
maendeleo ya Jimbo kupitia mfuko wa Mwakilishi wa Jimbo la Micheweni imepitisha
miradi mine ambayo itaanza kutekelezwa hivi karibuni.
Hatua hiyo
imekuja mara baada ya kumalizika kwa kikao cha kamati hiyo kilichofanyika leo
cha kujadili na kupitisha miradi mbalimbali ya maendeleo katika jimbo hilo.
Akizungumza katika
kikao hicho, Mwenyekiti wa kamati hiyo ambae pia ni mwakilishi wa jimbo hilo,
Mhe. SHAMATA SHAAME HAMIS amesema miradi hiyo ni moja ya vipaumbele ambavyo
vimechaguliwa na wananchi katika maeneo yao.
SHAMATA
amesema atahakikisha kwamba miradi yote iliyopitishwa na kamati hiyo
inatekelezwa kama ambayo imekusudiwa.
Katibu wa
kamati hiyo, Mwalimu MKASHA SHAAME, amesema kamati yao inaendelea kuhakikisha
kuwa miradi yote iliyopendekezwa na wananchi inatekelezwa ili kuwaondoshea wananchi
usumbufu.
Kwa upande wake mjumbe wa kamati hiyo Bi
SOPHIA MOHAMED MZIRAI, amesema amefurahishwa na ushirikishwaji wa wanawake
katika kamati hiyo na kujiona na wao wana nafasi ya kushiriki kupitisha miradi
mbalimbali ya maendeleo.
Katika kikao
hicho, miradi ambayo imepitishwa na kamati hiyo ni mapoja na, mradi wa Umeme
katika shehia ya Majenzi, Ukumbi wa Mikutano Skuli ya Kiuyu, Soko la Micheweni,
na visima katika Shehia ya Maziwang’ombe.
Post a Comment