MASHEHA TATUENI MIGOGORO KATIKA SHEHIA ZENU
Mkuu wa
wilaya ya Micheweni salama mbarok khatibu amewata wanashehia ya maziwa ngombe
na mjini wingwi kutofanya shughuli zao katika maeneo yenye mgogoro
Ameyasema
hayo wakati alipokuwa akizungumza na wazee wa pande mbili zenye mgogoro ili
kuweza kumaliza kwa njia ya amani katika
maeneo hayo
Amesema kila
mmoja anayestahili kupatiwa haki yake ameipata
kwani nia ya serekali nikuona wananchi wake wanaishi bila kuwa na
matatizo na mizozo katika maeneo yao
Salama
ameendeleea kuwaomba wazee hao kuwa elimisha vijana katika maeneo yao ili
kuweza kuondosha uhasama kwani wote ni wanafamilia moja
Naye mzee
khamisi Abdalla shame wa maziwa ngombe amesema tama ya mali ndio inayosababisha
kuwepo kwa mgogoro huo katika maeneo hayo ila kwao wanaona hakuna tatizo na wako tayari kumaliza tatizo hilo
Baraka
kutoka mjini wingwi amesema wao wako tayari serekali kwenda kuwaekeea mipaka
ili kuweza kuondo tatizo ambalo halina msingi na linapelekea kuwekeana hasama
katika shehia hizo mbili
Kikao hicho
ambacho kilikuwa kikiongozwa na mkuu wa wilaya ya Micheweni kimekubaniana
kuacha shughuli zao katika maeneo hayo mpaka serekali itakapo towa maelekezo
yake
Post a Comment