Header Ads

RC Kaskazini pemba ahimiza viongozi wa dini kuhubiri amani


Mkuu wa mkoa wa Kaskazini Pemba Mhe Omar Khamis Othman amewataka viongozi wa dini kuendelea kuhubiri amani ili kuwafanya wananchi  kupendana na kushirikiana katika masuala ya kujiletea maendeleo.

Amesema serikali imeweka mazingira mazuri ya wananchi wake kuabudu dini kila wanaotaka na kuwasisitiza kuhakikisha wanaitumia fursa hiyo kuhimiza amani na utulivu wa nchi.

Mhe omar ameyasema hayo wakati akizungumza na mchungaji wa Kanisa la Tanzania Assembles of  GOD –TAG-  lililoko Makangale Mchungaji   Samwel Elias   Maganga  ambapo amepongeza juhudi zinazochukuliwa na Kanisa hilo katika kusaidia huduma za kijamii.

Naye mchungaji wa Kanisa hilo Mchungaji Samwel  Elias Maganga amesema Kanisa limeandaa utaratibu wa kusaidia huduma za kijamii ikiwemo  masuala ya Elimu na michezo .

Aidha ameeleza kwamba  tayari jumla ya kaya 27 kutoka shehia ya Tondooni na Makangale zinanufaika na msaada wa chakula kila mwezi na familia 31 zimepatiwa mbuzi wa kufuga.

No comments