OPARESHENI DAWA ZA KULEVYA ZAMPAISHA DC MICHEWENI
WANASHEHIA ya Makangale na Kiuyu Kipangani wameipongeza kamati ya Ulinzi na Usalama kwa
juhudi za kupambana na watu ambao wanaingiza madawa ya kulevya, na pombe
katika maeneo yao.
Hatua hiyo imekuja
baada ya kamati hiyo kufanya oparesheni katika maeneo mabali
mbali ya wilaya hiyo na kukamada madumu 36 ya pombe za kienyeji pamoja na dawa za kulevya aina ya Bangi.
Akizungumza mara baada ya kufanyika kwa zoezi hilo, Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama, ambaye pia ni Mkuu
wa Wilaya ya Micheweni Salama MbarouK Khatib amesema kunabaadhi ya vijana
taayari wameathiriwa na dawa hizo na wanashindwa kufanya kazi
"Katika Oparesheni hii tumebaini kuwepo kwa kundi kubwa la vijana ambao tayari wameshakuwa 'Madondocha' hivyo kuprlrkra kushindwa kujishughulisha katika kazi za maendeleo," alisema Mkuu huyo wa Wilaya.
Aidha katika hatua nyingine, Salama amesema
kuna baadhi ya viongozi hawaungi mkono juhudi hizo ambazo wanazichua katika
kupambana na madawa ya kulevya na pombe za kienyeji.
kwa upande wake Said Shaibu Masoudi
mkazi wa Kipange amesema Serikali ya Wilaya ya Micheweni imewasaidia kwa kiasi
kikubwa kutokana na kuwatia mbaroni wale ambao wanajihusisha na pombe na madawa
ya kulevya.
Masoud amesema
maeneo yao yamekuwa kama sitendi ya kuingiza madawa na upikaji wa POMBE za
kienyeji na kusababisha vijana kulaitiwa na kufanywa kama wanawake.
Naye Ali Hamadi
Bakari amesema serekali ya wilaya ya Micheweni imejuwa wajibu wake wa kusimamia
vijana wake ili wasiharibike kwa kuvuta bangi na utumiajia wa Pombe haramu.
Post a Comment