Header Ads

VIJANA WA BOLINGO WAIBANA MBAVU NGORONGORO HEROES NYUMBANI

Timu ya Taifa ya Vijana chini ya mika 20, 'Ngorongoro Heroes' imelazimishwa suluhu ya 0-0 dhidi ya Congo katika mchezo wa kuwania fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON U20).

Katika mchezo huo uliopigwa jijini Dar es Salaam 'Uwanja wa Taifa' umemalizika bila kushuhudiwa nyavu zikitikisika.

Matokeo hayo yanakuwa ni mwanzo mbaya kwa Ngorongoro ambayo itacheza mchezo wa marudiano na Congo huko Kinshasa.

Ngorongoro wataanza maandalizi mengine kwa ajili ya kurudiana na Congo baada ya wiki mbili zijazo.

No comments