Header Ads

'UGATUZI WA MADARAKA UMELETA MABADILIKO KIUTENDAJI'




Ziara ya kamati ya afya , mazingira na ustawi wa jamii ya baraza la mji wete imebaini kuwepo na mabadiliko makubwa ya upatikanaji wa huduma za kijamii baada ya mfumo wa ugatuzi kufanyika kwa baadhi ya wizara .
 
Mwenyekiti wa kamati hiyo SAID KHAMIS MOHAMMED amesema katika ziara hiyo watumishi wa serikali wameelezea kuridhishwa na mfumo huo ambao umesaidia kupatikana kwa huduma muhimu kwa wakati.
Amesema mfumo huo pia umewaweka karibu na taasisi ya baraza la mji , na kwamba mawasiliano yameimarika na watumishi huwasiliana na moja kwa moja na uongozi wa baraza kupata ufumbuzi wa changamoto zinazowakabili .
Naye afisa elimu na mafunzo ya amal wilaya ya wete khamis said hamad amesema mfumo wa ugatuzi umewaweza wananchi kuwa karibu na wizara ya elimu .
Amesema hata ongezeko la wanafunzi walioandikishwa pia limechangiwa na mfumo wa ugatuzi ambapo wazazi na walimu wamekuwa na ushirikiano wa karibu .
Amesema mfumo huo umewawezesha wanajamii kushiriki kusimamia maendeleo ya elimu katika shehia zao na hivyo kurahisha upatinaji wa wanafunzi .
Na Massanja Mabula

No comments