Mh. Samia Suluhu Aridhishwa na Amani iliyopo Kisiwani Pemba
MAKAMO wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema Serikali imeweka mkazo maalum katika
kuimarisha huduma za afya hasa za
mama na mtoto ili kupunguza vifo vinavyotokea wakati wa kujifungua.
Makamo wa Rais ameyasema hayo huko Shehia Shumba Vyamboni katika Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba wakati alipokuwa akizungumza na wananchi mara baada ya kuweka jiwe na msingi katika kituo cha afya cha huduma za mama na mtoto .
Amesema kwa makisio
kila mwaka akina mama mia nne kati ya laki moja hupoteza maisha kwa sababu mbali mbali zitokianazo na
uzazi moja wapo ni kuchelewa
kufikishwa katika vituo vha afya na hospitali.
Aidha amewataka
wananchi wa shehia hiyo kukitumia kituo hicho pamoja na kuilinda miundo mbinu yake ili kiweze kudumu na
kutumika kwa muda mrefu kama
ilivyokusudiwa na kiweze kutoa huduma bora kwa manufaa ya umma.
Mapema akimkabirisha
Makamo wa Rais , Waziri wa Nchi . Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Zanzibar Mohammed Abod Mohammed
amesema miongoni mwa mikakati ya
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ni kuimarisha huduma za afya kwa wananchi wake.
Aidha amefahamisha kwamba
ujenzi wa Kituo hicho ni moja ya malengo la Mapinduzi ya Zanzibar ya kuhakikisha kwamba kila
mwananchi ananufaika na matunda
yake ambapo kituo hicho ni moja ya matunda ya Mapinduzi .
“Moja ya malengo ya
matunda ya Mapinduzi ya Januari 1964 ni kuhakikisha
wananchi wa Zanzibar wananufaika na huduma bora za afya , kwamba ujenzi wa kituo hichi ni utekelezaji wa azma ya
Mapinduzi hayo
”alifahamisha.
”alifahamisha.
Wakati huo huo ,
Makamo wa Rais pia amemtembelea mwasisi wa Chama Cha Mapinduzi Mrashi Seif Khamis huko Shehia ya Sizini na
kukabidhi msaada wa mabati kwa
ajili ya kuezeka nyumba yake iliyojengwa kwa mchango wa wanaCCM wa Wilaya ya Micheweni.
Pia Makamo wa Rais amepata
fursa ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa Tawi
la CCM Shehia ya Ukunjwi Wilaya ya Wete na kuwapongeza wanaCCM kwa kuendelea kudumisha umoja na mshikamano.
MATUKIO KATIKA PICHA
PICHA ZOTE NA (GASPARY CHARLES)
Post a Comment