'Viongozi wa Dini Hubirini na Kukemea Haya'- Rais JPM
Rais John Magufuli amewataka Wahubiri na Maaskofu
nchini Tanzania kwa pamoja kuliombea na Taifa na kuwashawishi wananchi wake
suala zima la kutambua umuhimu wa kujenga viwanda vya madawa ili kuweza
kuzalisha bidhaa zake na kuwapatia vijana ajira.
Dkt.
Magufuli ametoa kauli hiyo leo (Machi 26, 2018) wakati alipokuwa anafanya
uzinduzi wa magari mapya 181 ya kusambaza dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya
maabara eneo la Keko Jijini Dar es Salaam.
"Uchumi
wa Viwanda hauwezi kufikiwa bila kuimarisha sekta ya afya, tunatenga bilioni
260 kununua dawa lakini ni 6% tu ndiyo zinanunuliwa ndani. Tengenezeni
njia ya kupata wawekezaji watakaojenga viwanda vya dawa na vifaa tiba hapa
nchini, sijui watanzania tumerogwa au shetani amekaa mno hapa, basi tumkemee kwa
majina yote akashindwe...
Ili
kusudi watanzania tujue ni namna gani tunatakiwa kwa kupata fedha. Niwaombe
Maaskofu walihubiri na kulikemea hili na watu wengine wanaojua kuhubiri
vizuri tuwaeleza watanzania kwamba tunapoteza bilioni 500 kila mwaka kununua
madawa wakati tungekuwa tunatengeneza nchini zingebaki hapa,tunalalamikia
mengine yale ya maana ya kuyalalamikia hatuyapigii kelele", amesema
Dkt. Magufuli.
Pamoja na hayo, Rais Magufuli ameendelea kwa kusema "kusubiri ni kugumu, tutengeneze njia sasa, Wizara ya Afya
kaeni na wafanyabiashara wa ndani muone namna ya kuwawezesha wafungue viwanda
vya dawa. Tuwakusanye pia mafamasia wetu tuone namna ya kuwawezesha kufungua
viwanda, na majeshi yetu pia. Nasikia mnakwamishana wenyewe hapa, TFDA
wanazuia dawa zenu bandarini na wakati mwengine mpaka zina-expire. akizuia tena
niambieni halafu nione nani huyo mwenye mamlaka zaidi yangu".
Kwa upande mwingine, Mkurugenzi Mtendaji wa MSD
Laurian Bwanakunu amesema baada ya kuongezewa bajeti yao kufikia bilioni 250
kwa sasa MSD wanasambaza dawa zenye thamani ya bilioni 18 na lengo ni kufikia
bilioni 21 ikifika mwezi Julai.
Post a Comment