Moto uliozuka jumba la Kemerovo, Urusi wawaua watu 53

Baadhi ya maeneo ya jumba hilo kubwa yanadaiwa kuwa kwenye hatari ya kuporomoka.
Moto huo ulianza katika ghorofa ya juu katika jumba Winter Cherry.
Inadaiwa wengi wa waliofariki walikuwa kwenye kumbi za sinema.
Video zililoonyeshwa mitandao ya kijamii zinawaonesha watu wakiruka
nje kupitia madirisha kujaribu kujinusuru kutoka kwa moto huo uliozuka
Jumapili.
Wazima moto zaidi ya 660 wametumwa kusaidia juhudi za uokoaji.
Chanzo cha moto huo hakijabainika lakini maafisa wameanzisha uchunguzi.
Post a Comment