Dkt. Maria Kamm mwanamke wa kwanza kupata Degree Tanzania
Dkt. Maria Kamm ndiye mwanamke wa kwanza wa Tanzania kupata Shahada
ya kwanza (Degree) na leo ametunukiwa tuzo ya heshima katika tuzo za
Malkia wa Nguvu zinazoandaliwa na Clouds Media.
Mama Kamm ambaye aliwahi kuwa Mkuu wa Shule ya Sekondari
ya Weruweru iliyopo Mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro, akiwa kama Mzalendo
wa kweli, ametumia maisha yake kwa kiasi kikubwa kuwashauri na
kuwaelimisha vijana katika masuala mbalimbali ya Taifa.
Mgeni Rasmi katika utoaji wa Tuzo hizo uliofanyika katika Ukumbi wa
Mikutano wa Mwl Nyerere Posta jijini Dar, alikuwa Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto, dkt. ummy Ally Mwalimu.
Post a Comment