RUSHWA MUHALI, SULUHU KESI ZA UDHALILISHAJI ZAPIGWA MARUFUKU
WARATIBU
wa wanawake na watoto wilaya ya wete wametakiwa kuacha rushwa muhali pamoja na
kujiepusha na kushiriki kufanya suluhu juu ya matendo ya udhalilishaji
yanapotokea katika maeneo yao.
Katibu
Tawala Wilaya ya Wete Bi Mkufu Faki Ali akizungumza na waratibu amesema
Serikali imekusudia kuyatokomeza matendo hayo , hivyo ni jukumu la waratibu
kusimamia na kutoa taarifa sahihi na za mapema yanapotokea katika shehia zao.
Amewataka
waratibu kuhakikisha kesi zote za udhalilishaji zinar ipotiwa sehemu
husika ili wahusika waweze kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria za nchi .
Naye Afisa
Ustawi wa Jamii wilaya hiyo Haroub Suleiman Hemed amesema baadhi ya waratibu
wanashiriki kufanya suluhu ya matendo hayo na baada ya akushindwa kufikia
makubaliano kesi hizo huziripoti sehemu husika kwa hatua za kisheria.
Haroub
amefahamisha kwamba kesi nyingi zinazotokea hasa maeneo ya vijijini hushindwa
kuripotiwa sehemu husika na badala yake waratibu kushiriki kuzipatia suluhu
jambo ambalo ni kosa kisheria.
Washiriki wa
kikao hicho wameishauri jamii kushirikiana katika kupiga vita matendo hayo ambayo
yanazidi kushamiri katika Mkoa wa Kaskazini Pemba hususani wilaya ya wete.
Post a Comment