RC KUSINI PEMBA: VIJANA SOMENI HISTORIA YA NCHI KUJUA UKWELI WA MAMBO
Mkuu Wa Mkoa Wa Kusini Pemba Hemed Suleiman Abdalla
amewataka vijana kisiwani Pemba kuisoma vyema historia ya nchii ili kufahamu
ukweli pamoja na kutambua ukombozi mkubwa walioupata kutoka kwa hayati
Mzee Abedi Amani Karume.
Ameyasema hayo wakati alipokuwa akifungua kongamano LA kumbukumbu
ya kumuenzi hayati Mzee Abedi Aman karume lililowashirikisha vijana kutoka
baraza LA vijana chakechake huko katrika ,ukumibi Wa Tasaf Pemba.
Amesema vijana watakapoielewa vyema historia watakuwa mabalozi
wazuri kwawenzao pamoja na kueleza ukweli unaopigwa na baadhi ya makundi
ya watu.
Mapema Mkuu Wa Wilaya ya chake chake Rashid Hadidi R
ashidi Amesema wanakila sababu ya kumkumbuka na kumuezi Hayati Karume
kwani amewakomboa katika ukoloni Wa kisultan na kuwafanya wawe huru.
Nae Mwenyekiti Wa baraza LA vijana la chake chake Bakar
Hamad Bakar amesema wapo tayari kuyalinda kuyaenzi na kuyatetea Mapinduzi ya
Zanzibar kwakila hali kwanii wanakila sababu ya kufanya hivyo.
Post a Comment