Juhudi kuanza kuchukuliwa uboreshaji Elimu Skuli ya Kizimbani Sekondari
UONGOZI
wa Skuli ya kizimbani sekondari umeanza mikakati ya kuinua kiwango cha ufaulu
wa wanafunzi wa kike wa kidato cha nne , kwa kuwaandalia mzaingira mazuri ya
kujifunza pamoja na kuwahamasisha wazazi kushirikiana na walimu
kufuatilia maendeleo ya watoto wao.
Hayo
yamesemwa na mwalimu mkuu wa skuli hiyo Bisabahi Mussa Said wakati
akizungumza na uongozi wa chama cha mapinduzi CCM Jimbo la gando waliofanya
ziara ya kutembelea miradi ya serikali katika jimbo hilo .
Mwalimu
Mkuu wa skuli hiyo Bi Sabah Mussa Said amesema uongozi wa skuli umechukizwa
sana na kitendo cha wanafunzi wa kike kufanya vibaya kwenye mitihani ya ya
kidato cha nne .
"Mwaka
jana wanafunzi wa kike waliofaaulu kuendelea na masomo ya kidato cha tani
walikuwa wengi kuliko wanaume , hivyo matokeo ya mwaka huu yametuchanganya
walimu ‘’ alisema .
Aidha
amesema kuwa moja ya sababu ambazo zimesababisha matokeo hayo ni kwa baadhi ya
wazazi kutokuwa tayari kushirikiana na walimu pamoja na kamati ya skuli katika
kufuatilia maendeleo ya watoto wao.
Mwenyekiti
wa CCM jimbo la Gando Massoud Ismail Juma amesema lengo la ziara hiyo ni
kuangalia utekelezaji wa ilani ya chama pamoja na kufuatilia ahadi za viongozi
.
Mwakilishi
wa jimbo la Gando Maryam Than Juma amewataka walimu kuwa karibu na wazazi
kuendelea kushirikiana ili kuwafanya wanafunzi kuongeza uwezo wao kielimu .
Mariam
amesema utaratibu wa zamani wa kila mwanafunzi mtoro kuitwa skuli pamoja na
mzazi wake unafaa kurejeshwa kwani ni moja ya utaratibu uliokuwa unasaidia
wanafunzi kufuatilia masomo yao darasani.
Post a Comment