ZAECA Wafunga Ghala la Chakula Wete
MAMLAKA
ya kuzuia Rushwa na Uhujumu wa Uchumi Zanzibar –ZAECA- Mkoa wa Kaskazini Pemba
imefunga ghala la kuhifadhia chakula katika Bandari ya Wete ili kuendeleza zuio
la kutotumika mafuta ya kula yaliyohifadhiwa ndani ya ghala hilo.
Mdhamini
wa Mamlaka hiyo Mkoa wa Kaskazini Pemba Abubakar Mohammed Lunda amesema ZAECA
imechukua uwamuzi huo baada ya kubaini kuwa mafuta hayo hayafai kwa matumizi ya
binadamu .
Ameeleza
kuwa mafuta hayo aina ya HAYATI na TASTY TOM yalikamatwa yaliingiza
kinyume na sheria , na kuzuiwa yasitumike ambapo ZAECA ililazimika
kuchukua sampuli kupeleka kwenye maabara ambapo majibu yametolewa kwamba
hayafai kwa matumizi .
Katika
maelezo yake Abubakar amesema kuwa ghala hilo amelifunga na kwamba wakala
akihitaji bidhaa atawasiliana na Mamlaka kwa ajili ya kufunguliwa .
‘’Mamlaka
imelazimika kuchukua uwamuzi wa kulifunga ghala hili ili kuzuia mafuta yaliyomo
ndani yasiendelee kuuzwa kwani hayafai kwa matumizi ya binadamu ‘’ .
Aidha
Abubakar ameeleza kwamba wamemuandikia barua mmiliki wa mafuta hayo Ali Shaib ,
na hatua za kisheria zinafuata ikiwa ni pamoja na kumfikisha mahakamani kujibu
tuhuma za kuuza bidhaa ambazo haifai kuliwa .
Abubakar
amewataka wananchi kuwa makini wanaponunua mafuta ya kula kwa kuangalia muda
wake wa matumizi ili kuepuka kupata aradhi .
Wakala
wa mfanyabiashara aliyeingiza mafuta hayo , amesema kuwa uwamuzi wa kuendelea
kuyauza baada ya kupokea barua kutoka Taasisi ya Viwango Zanzibar –ZBS-
kwamba mafuta hayo yanafaa kwa matumizi .
Amesema
kuwa awali alipokea barua inayomtaka kuzuia kuyauza mafuta hayo na alitii ,
lakini baada ya kupata idhini kutoka ZBS akaamua kuendelea kuyauza mafuta .
Post a Comment