'KAMBARE HATARINI KUTOWEKA ZIWA MAKANGALE'
WAKAAZI wa shehia
ya Tondooni na Makangale Wilaya ya Micheweni wamesema kwamba mabadiliko ya tabianchi yameanza
kutishia kutoweka samaki aina ya Kambare wanaopatikana kwenye ziwa Makangale .
Wamesema samaki hao
ni moja ya kitoweyo kinachopendwa na wananchi wengi,kwa sasa upatikanaji wake umekuwa adimu kutokana
na Maji ya Bahari kuingia ndani ya ziwa Makangale na kusababisha samaki hao kutoweka.
Katika nasaha zake
kwa wananchi hao , Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Omar Khamis Othman ameahidi
kufanya ziara ya kulitembelea ziwa hilo , huku akiwa amefuatana na wataalamu wa
Kilimo , Misitu na Mazingira .
Ameeleza kwamba
ziara hiyo ambayo ataifanya pia utawahusisha wanajamii wanaozunguka ziwa hilo
ambao watahirikiana na wataalamu wa kilimo na Mazingira kutafuta ufumbuzi wa
changamoto hiyo ya maji ya chumvi kuvamia ziwa hilo.
Post a Comment