MADIWANI BARAZA LA MJI WETE WAGOMA KUPITISHA BAJETI 2018/19
Madiwani wa Baraza la
mji Wete wamekataa kuipisha Bajeti ya mwaka 2018-2019 kwa madai kuwa ni ndogo
kulingana na vyanzo vya mapato vilivyomo katika baraza hil.
Baraza hilo limepanga
kukusanya shilingi milioni 270,000,000/=kwa
mwaka 2018-2019.
Wakizungumza
kwenye kikao hicho madiwani wamehoji uhalali uliotumika kuweka makadirio hayo ,
huku wakisema hakuna tofauti iliyozingatiwa katika kuweka viwango vya
leseni kwa maduka .
Diwani
wa kuteuliwa Zulfa Abdalla Said amesema bajeti hiyo iliyokadiriwa haina
uwiano wa leseni za maduka kwa wafanyabiashara wadogo ,wa kati na wakubwa .
Kaimu Mkurugenzi wa Baraza hilo Bi Salma Abuu
Hamad amesema kamati ya fedha imeandaa utaratibu wa kuwatumia madiwani katika
maeneo yao kuyabaini maduka .
Mwenyeketi wa kamati
ya fedha akawashukuru madiwani licha ya kutoipisha bajeti hiyo .
Post a Comment