DC MICHEWENI: VIJANA DHIBITINI MIHEMUKO YA MIILI YENU
MKUU wa Wilaya ya
Micheweni Bi Salama Mbarouk Khatib amewataka vijana kudhibiti mihemko ya miili yao kwa kutambua
thamani yao ili kuzuia mimba za umri mdogo pamoja na vitendo vyengine vya
udhalilishaji.
Amesema vitendo vya
udhalilishaji vinavyotokea siku hadi siku vinachangiwa na baadhi ya vijana kushindwa kuidhibiti mihemko na hivyo
kufanya maamuzi yasiyo sahihi juu ya maisha yao .
Hayo yameelezwa na
Afisa wa Wanawake Wilaya hiyo Bizume
Haji Zume kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya , wakati akifungua kongamano la kupinga
mimba za utotoni pamoja na vitendo vya udhalilishaji lililofanyika kwenye
ukumbi wa Skuli ya Sekondari ya Micheweni.
Amefahamisha kwamba wanakabiliwa na changamoto
nyingi ikiwemo ya utumiaji wa dawa za kulevya , ubakaji pamoja na wizi , hivyo
wanapaswa kupunguza mihemko kwa faida yao na jamii kwa ujumla.
Naye Afisa Vijana
Wilaya ya Chake Chake Omar Abeid Ali amewataka vijana kujitambua na kujiepusha na
vikundi viovu ambavyo vinaweza kuleta athari katika maisha yao .
Post a Comment