Korea Kusini na Korea Kaskazini zafungua njia ya simu ya mawasiliano ya moja kwa moja kati ya viongozi wa nchi hizo

Korea
Kusini na Korea Kaskazini zimefungua njia ya simu kwa mawasiliano ya moja kwa
moja kati ya viongozi wa nchi hizo mbili.
Mkurugenzi
wa idara ya serikali katika Ikulu ya Korea Kusini Yun Kun-young amesema, njia
hiyo ya simu imeunganishwa kati ya ikulu ya Korea Kusini na Kamati ya Masuala
ya Kitaifa ya Korea Kaskazini.
Rais
Moon Jae-in wa Korea Kusini na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un walikubaliana
kufanya maongezi yao ya kwanza kwa njia ya simu kabla ya kufanya mkutano wao wa
kwanza tarehe 27 mwezi huu katika kijiji cha mpakani cha Panmunjom.
Post a Comment