Umoja wa Afrika wazitaka pande mbalimbali za Sudan Kusini kutimiza ahadi ya mchakato wa amani
Ujumbe
wa baraza la amani na usalama la Umoja wa Afrika PSC umemaliza majukumu yake ya
siku sita nchini Sudan Kusini, ukizitaka pande zote zinazopambana kutimiza
ahadi yao kwa mchakato wa amani unaoendelea.
Ujumbe
huo pia umeziaka pande husika kufikiria makubaliano halisi ya amani na
kuhakikisha duru ijayo ya mazungumzo ya baraza la HLRF isishindwe kwa kuwa ni
fursa ya mwisho kwa amani.
Ujumbe
huo umetoa taarifa kuwa ujumbe wa PSC unawahakikishia wadau wote utayari na
dhamira ya Umoja wa Afrika ya kufanya juhudi zote katika kuunga mkono IGAD na
pande mbalimbali za Sudan Kusini kutatua changamoto zinazoukabili mchakato wa
amani.
Post a Comment