Header Ads

NUSU FAINALI ASFC HAPATOSHI LEO KAMBARAGE STAND UNITED vs MTIBWA SUGAR


Image result for KOMBE LA SHIRIKISHO ASFCNUSU Fainali ya kwanza ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) inatarajiwa kufanyika leo Uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga ikizikutanisha wenyeji, Stand United na Mtibwa Sugar ya Morogoro.

Kocha wa Mtibwa Sugar, Zuberi Katwila ni mwenye matumaini makubwa kuelekea kwenye mchezo hyo, akiamimi timu yake itawafunga wenyeji na kwenda Fainali ya michuano hiyo kwa mara ya kwanza katika historia yao.

Katwila amesema kwamba wachezaji wote muhimu wa Mtibwa Sugar wako fiti na tayari kwa mchezo wa leo, akiwemo kiungo Hassan Dilunga ambaye alikuwa majeruhi.

Nusu Fainali ya pili Azam Sports Federation Cup itafuatia Jumatatu Uwanja wa Namfua mjini Singida, ikizikutanisha JKT Tanzania ya Dar es Salaam na wenyeji Singida United.

Fainali ya michuano hiyo itafanyika Juni 2, mwaka huu Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha na bingwa pamoja na kupata Sh. Milioni 50, pia ataiwakilisha Tanzania kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Mshindi wa pili atapata Milioni 10, wakati Mchezaji Bora atazawadiwa Sh. Milioni 1 sawa na Kipa Bora, Mfungaji Bora, huku Mchezaji Bora wa Fainali akiondoka na Sh. 500,000. 

No comments