Sh1.5 Trilioni zinazodaiwa kutojulikana zilipo, Serikali yatolea ufafanuzi

Hayo yamesemwa na Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt Ashatu Kijaji mapema leo bungeni alipokuwa
akitoa tamko la serikali kuhusu fedha shilingi trilioni 1.51 zinazodaiwa
kutumika bila kuwepo kwa maeneo ya namna zilivyotumika.
Dkt Kijaji amesema kuwa, wale
wote wanaozusha kuwa kuna fedha zilitumika bila kuwa na maelezo, hawalitakii
mema taifa pamoja na serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Pombe
Joseph Magufuli.
Akitoa mchanganuo wa matumizi
wa fedha hizo Dkt Kijaji alisema, fedha trilioni 1.51 zinazodaiwa
kutoonekana kwenye matumizi ya serikali zimetoka na matumizi ya dhamana na hati
fungani zilizoiva TZS trilioni 0.6979, mapato tarajiwa TZS trilioni 0.6873,
mapato ya kodi yaliyokusanywa kwa niaba ya #ZanzibarTZS trilioni 0.2039. Jumla ya fedha
zote hapa inakuwa ni TZS trilioni 1.5891.
Fedha iliyotolewa zaidi ya
mapato (Bank Overdraft) ni TZS trilioni 0.0791, na hivyo kufanya kusalia kwa
TZS trilioni 1.51 inayodaiwa kutoonekana kwenye matumizi ya serikali.
Post a Comment