Sakata la vijana U-17 'KARUME BOYS', ZFA wasema watajiuzulu
Kauli hiyo
ilitolewa na Makamu wa Rais wa ZFA Pemba, Ali Mohammed ambaye alikuwa meneja wa
timu hiyo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari huko Amaan jana.
Alisema, ZFA
haina muongozo wowote uliotumwa kwao kuhusu umri au tarehe iliyotakiwa kwa
ajili ya kwenda Burundi na kusema wapo tayari kutoa barua pepe zote mbili
ikiwemo ya ZFA na Makamu wa Rais Unguja pamoja na namba za siri kwa wataalamu
wa mitandao ili kuzikagua kwa kina kama kweli walitumiwa.
“Tumekuja hapa
kusema kwamba ZFA haina ‘toleo’ lolote lililotumwa na CECAFA kwa ajili ya
kuelezea umri au tarehe ya umri iliyotakiwa kwenda Burundi”.
“Tunatoa wito kwa
wataalamu wa mitandao kuja ili tuwakabidhi ‘ barua pepe’zetu wazifanyie kazi
kwa mujibu wa utaalamu wao, wakiliona hilo tupo tayari kuwajibika hata leo”,
alisema.
Hata hivyo,
alisema, pamoja na kwamba wameondolewa kuna hatua wanazozichukua kwa sababu
hawajaridhika na sababu za kwenye barua za kuondolewa kwao.
“Karume Boys
imeondoshwa na kuna hatua tunazichukuwa, moja ni kukata rufaa ambayo tumeianza
juzi. Jambo la pili tumejiridhisha kwamba hatuna ‘toleo’ la aina yoyote
inayotoa tafsiri ya U-17”, alieleza.
Alisema
mashindano hayo yanaitwa U-17 na ndio kanuni za CECAFA zinavyosema katika
kifungu cha nne, ambayo haina tafsiri ya U-17 ,lakini, kwa uzoefu wa ZFA
tuliona watu wote ambao hawajafikia umri wa miaka 17.
“Ninachojua mimi
na ZFA tafsiri yetu sahihi ilikuwa hii na mtakumbuka kwamba timu hiyo iliitwa
kambini mwezi wa tatu na kulijitokeza wachezaji waliokuwa na umri mkubwa kabla
ya timu hiyo kuvunjwa”.
“Baada ya kuundwa
nyengine ambayo nayo watu waliiona ya kufungwa kutokana umri wa watoto ambao
tumewapeleka, alisema.
Aidha, alisema,
kabla ya kuipelekea timu hiyo walipokea barua pepe kutoka CECAFA ya kuwataka
watume majina, paspoti namba na tarehe za kuzaliwa kwa wachezaji watakaoshiriki
mashindano hayo kwa ajili ya kuthibitishwa.
Alisema, mnamo
Aprili 7 mwaka huu, walituma majina hayo kwa kufuata maagizo na Aprili 11 saa
5:30 za usiku walitumiwa tiketi kwamba wameridhika na wao kama ZFA walifarijika
na kusafiri kwenda Burundi.
Alisema, Zanzibar
katika mashindano hayo walipangwa katika kituo cha Itega pamoja na Sudan,
Ethiopia na Tanzania ambapo kwa bahati nzuri timu zote zilikutana katika uwanja
wa Ndege na nchi ya mwanzo kuanza kulalamika ilikuwa Sudan ambayo ilisema
katika timu zote ambazo zimetuma wachezaji wadogo ni Zanzibar pekee.
Lakini hatukwenda
tu, CECAFA ilisema wachezaji wote ambao watakwenda ni lazima wawe wamefanyiwa
kipimo cha MRI ambacho kitakuwa ni kithibitisho na kuchukuliwa Burundi, alisema.
Hata hivyo,
alisema, hayo pia Nicolus Musonye hakuwatumia bali walipata maelekezo kutoka
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupitia Alfred Kidau ambae alimpigia simu
Makamu wa ZFA Unguja Mzee Zam Ali na kumuelekeza utaratibu uliopo kuhusu kipimo
hicho.
Alisema mnamo
tarehe 15 Aprili saa 9:30 za Burundi walikwenda katika mechi na wao ndio
waliokuwa wa mwanzo kuikagua Sudan na kugundua kuna wachezaji wanne waliozidi
umri na kuzuia pasi zao kabla ya nahodha wa Sudan naye kuwakagua na kuridhika
na wachezaji wote.
Post a Comment