Header Ads

Makamo wa Pili wa Rais: 'Wafugaji,wakulima acheni kufanya kazi kwa Mazoea, Fanyeni kwa Malengo


Image result for Balozi Seif Ali Iddi 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema   wakati umefika kwa Wafugaji wa Samaki na Mazao mengine ya Baharini Nchini kubadilika kufanya kazi kwa mazoea ya kupata kitoeo tu, bali wafuge Kibiashara kwa lengo la  kuongeza uzalishaji wa samaki ili kuinua Sekta ya Uvuvi kwa maslahi binafsi, Jamii na Taifa.

Balozi Seif Ali Iddi ameyasema   hayo wakati wa hafla ya ufunguzi wa Kituo cha Utotoaji wa Vifaranga vya Samaki {Marine Hatchery} kilichojengwa pembezoni mwa Kampasi ya SUZA iliyopo Beit - El Ras nje kidogo ya Kaskazini  ya Mji wa Zanzibar.

aidha  mh  Balozi Seif  amefahamisha kwamba mradi wa kutotoa vifaranga vya samaki na mazo mengine ya Baharini umeanzishwa kwa lengo la kupanua wigo wa shughuli za ufugaji wa samaki ili Wananchi waweze kuwa na sehemu maalum ya kupata vifaranga vya kutosheleza na vyenye ubora unaohitajika.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliiagiza Wizara ya Kilimo, Mali asili, Mifugo na Uvuvi kuwaandalia mazingira bora Wananchi wa Unguja na Pemba yatakayowawezesha kupata vifaranga hivyo kwa urahisi.

Amesema takwimu zinaonysha kuwa zibar hivi sasa ina zaidi ya Vikundi 144 viavyojishughulisha na harakati za ufugaji wa samaki ambapo vikundi vyote hivyo hutegemea vifaranga kutoka nje ya Zanzibar ambavyo havina uhakika wa ubora na upatikanaji wake.

Alieleza kuwa uzinduzi wa Kituo cha Kutotolea Vifaranga vya Samaki na Mazao ya Baharini  cha Beit – El Ras utakuwa ni ufumbuzi wa changamoto iliyopo kwa Wafugaji wa samaki Nchini hasa katika  upatikanaji wa vifaranga kwa uhakika ambapo kwa sasa wataweza kuzalisha samaki kwa wingi na kujiongezea kipato.

Alifahamisha kwamba zaidi ya asilimia 50% ya vyakula vyote vya Baharini {SEAFOOD} vinavyotumiwa Duniani hivi sasa vinatokana na ufugaji, hivyo maeneo ya hifadhi za Bahari ni vyanzo muhimu vya mazalia ya samaki yanayopaswa kupatiwa hifadhi ya msingi.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwaomba Wananchi kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika uhifadhi wa mazingira ya Bahari kwa faida yao na vizazi vijavyo.

 Mapema akitoa Taarifa Katibu Mkuu  Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Bibi Marya Abdulla Juma alisema Kituo hicho cha utotoaji wa Vifaranga vya Samaki ni za Barani Afrika  ni cha kwanza cha kumi duniani .

 Amesema chuo  otoaji wa vifaranga vya samaki Beit el ras kinatarajiwa kuzalisha vifaranga 10,000 vya samaki, Kaa 75 pamoja na Majongoo 55 ili baadae kusambaza kwa wafugaji wa mazao hayo ya baharini.

Akitoa salamu Rais wa Shirika la Kimataifa la Misaada ya Maendeleo ya Korea {KOICA} Bibi Mikyung Lee aliipongeza Zanzibar kwa kupunguza ukali wa maisha kutokana na kupiga hatua kubwa za Maendeleo ikiwemo Sekta ya Viwanda.

Mradi huo wa Kituo Maalum cha Utotoaji Vifaranga vya Samaki Zanzibar uliogharamiwa na Shirika la Misaada ya Maendeleo la Korea {KOICA}kwa zaidi ya Dola za Kimarekani Milioni 3.2 unasimamiwa na kuendeshwa na Wataalamu wa Shirika la Kimataifa la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa {FAO}.

No comments