ZAWA yawomba radhi Wananchi, Yasema Tatizo la Upatikanaji wa Maji Safi na Salama linarekebishwa
Afisa uhusiano
kutoka Mamlaka ya maji Zanzibar
(ZAWA) amewataka wananchi wa shehia
ya pete kuwa wavumilivu kutokana na
tatizo la ukosefu wa maji safi
na salama kijiji hapo.
Ameyasema hayo Afisa
uhusiano mamlaka ya maji Zanzibar (zawa)
zahro Suleiman kufuatia malalamiko
yaliojitokeza kwa wananchi kutokana kwa
kukosekana huduma hiyo muhimu katika katika
shehia hiyo.
Amesema kwa
sasa wamejipanga kufanya marekebisho
katika kisima cha maji kiliopo unguja
ukuu kwa lengo la kuwapatia
wananchi huduma hiyo.
Kwa upande wa sheha wa
hiyo zakia mbaraka haji amekiri kuwepo
tatizo hilo na amesema limeshafikishwa sehemu
husika kwa ajili ya kupatiwa
ufumbuzi pia amezungumzia suala la watoto wanaotoka katika kijiji cha
pete na kufuata skuli huko Mtulee.
Nae mkazi wa eneo hilo hakupenda jina
lake litajwe amesema maji wanayotumia
kwa sasa ni ya kisima yanayotokana na
nguvu za wananchi wenyewe .
Pamoja na hayo
mamlaka ya maji zawa imewataka wananchi kuwa wastahamilivu kwa
kipindi cha miezi 3 ili kupatiwa ufumbuzi
wa tatizo hilo.
Post a Comment