Makazi ya Kudumu kikwazo kwa Wajasiriamali PEMBA
WAZIRI
wa Afya mhe HAMAD RASHID MOHAMMED amewataka Wajasiriamali Kisiwani Pemba kuwa
na utamaduni wa kurejesha mapato na matumizi kwa Wanachama wao ili kuondoa
malalamiko kuhusiana na mapato ya jumuiya Zao
Akifunga
mafunzo kwa wajasiriamali yaliyofanyika kwenye ofisi za umati Na malezi bora
tanzania zilizoko wete , mhe hamad amewasisitiza Viongozi wa vikundi hivyo kuwa
wawazi kwa wanachama wao kwa kutoa Taarifa za mapato na matumizi kwa wakati .
Naye
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo ya Elimu Zanzibar (ZEDO) USSI SAID
SULEIMAN amesema pamoja na jumuiya hiyo kupata mafanikio lakini
wanakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo ukosefu wa Ofisi ya kidumu
Mwezeshaji
wa mafunzo hayo , BI SUHY-ILA SALUM AMANI amesema zedo ni Mkombozi wa
wajasiriamali hususani vijana .
Mapema
akifungua mafunzo hayo , mwakilishi wa jimbo la Gando Mhe MARIAM THAN JUMA amesema
elimu ni jambo la lazima katika shughuli zawajasiriamali .
Post a Comment